News

Semina ya Mawasiliano Singida

Idara ya Mawasiliano ya Tanzania Rift Valley Field imewataka viongozi wa makanisa katika Kanda za Kinampanda na Manyoni kutumia teknolojia ya kidijitali kama nyenzo ya kueneza Injili.

Learn more

Akizungumza mkoani Singida katika semina maalum ya mawasiliano, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Jimbo hilo, Ndugu Abraham William, amesema kuwa kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia duniani, ni muhimu kwa kanisa kuendana na mabadiliko hayo kwa kutumia mitandao ya kijamii kuwafikia watu wengi zaidi.

Amesema kuwa ulimwengu wa sasa umetawaliwa na teknolojia, hali inayorahisisha kuwafikia watu wa rika na maeneo mbalimbali kwa wakati mmoja, hivyo viongozi wa makanisa wanapaswa kuyafanyia kazi mafunzo waliyoyapata ili kuongeza ufanisi katika kazi ya utume.

Wakati huo huo, baadhi ya viongozi walioshiriki katika semina hiyo wameushukuru uongozi wa jimbo kwa kuandaa mafunzo hayo, wakisema kuwa yamewasaidia kuelewa namna sahihi ya kutumia mitandao ya kijamii katika kuhubiri Injili.

Wamesema awali walikuwa na mashaka juu ya matumizi ya mitandao katika kazi ya utume, kutokana na namna ambavyo mara nyingi hutumiwa vibaya na baadhi ya watumiaji, lakini kupitia mafunzo hayo wamepata mwanga mpya wa kufanya uinjilisti kwa njia ya kidijitali.

Semina hiyo ya siku tatu ililenga kuwajengea uwezo viongozi wa makanisa katika kufanya uinjilisti wa kidijitali, huku msisitizo mkubwa ukiwekwa katika kuendelea kujifunza na kuchunguza Maandiko Matakatifu kwa kutumia Biblia.

WhatsApp Image 2026-04-16 at 02.46.35
previous arrow
next arrow

Ziara ya muhazini wa NTUC katika jimbo la TRVF

Mhazini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania (NTUC), Elder Mathias Mavanza, amesema kuwa Kanisa la Mungu litaendelea kuwa imara hata linapopitia nyakati ngumu.

Learn more

Kauli hiyo ameitoa katika Kanisa la Waadventista Wasabato Manyoni, mkoani Singida, wakati wa ibada maalum ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa jukwaa la kisasa katika kanisa hilo.

Aidha, baadhi ya washiriki wa kanisa hilo wamesema kuwa kwa sasa wamepata utulivu na amani baada ya kupata ufafanuzi kutoka kwa kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa kanisa, tofauti na taarifa walizokuwa wakizisikia kupitia mitandao ya kijamii ambayo si rasmi.

Katika ziara yake ya siku mbili katika Kanda ya Manyoni, Elder Mavanza alitumia fursa hiyo kuwaelewesha washiriki kuhusu taarifa zilizokuwa zikisambaa mitandaoni zikidai kuwepo kwa ubadhirifu ndani ya Kanisa la Waadventista Wasabato.

Amesema kuwa wakati mwingine Shetani anaweza kuwatumia watu mbalimbali kujaribu kulichafua Kanisa, lakini amewahimiza waumini kuendelea kuwa na imani na mshikamano ndani ya kanisa.

WhatsApp Image 2026-04-16 at 02.54.22
previous arrow
next arrow

Uzinduzi wa OneVoice 27 Arusha

Katibu Mkuu wa Jimbo la TRVF, Mchungaji Paschal Gissa ametoa Wito kwa waumini na viongozi wa Makanisa mahalia katika Jimbo hilo kuanza kazi ya Uinjilisti katika Maeneo yao baada ya Uzinduzi wa Program ya One Voice27.

learn more

Akizungumza siku ya Uzinduzi huo, Mchungaji Gissa amesema kwa sasa ni wakati wa kuanza Kazi ya kutangaza injili ya Yesu kwa kila Mtu ili ifikapoMwaka 2027 watu wengi wawe wamebatizwa kila Mahali kwasababu ana amini ujumbe wa One Voice27 utakua  umemfika sehemi mbali mbali.

Wakati huo huo baadhi ya waumini walioshiriki katika uzinduzi huo wamesema, uzinduzi wa One Voice27 umekua ni chachu ya kuamsha Kazi ya Mungu katika Jimbo la TRVF na wamepokea jukumu la kuanza kupeleka Habari njema za Yesu kwa kila mtu ili neno la Bwana limfikie kila Mmoja popote alipo.

Mwaka 2027 waumini wa Kanisa La Waadventista Wasabato Nchini Watasherehekea Miaka 2000 ya Yesu Kristo kubatizwa na TRVF wameamua kuzindua kazi ya Utume ya kumfikia kila mmoja na kumtangazia habari njema za Yesu Kristo, kazi iliyopewa jina la One Voice27.

IMG-20260420-WA0094
previous arrow
next arrow